NGO report

Swahili : Tanzania: Adhabu ya Kifo Imerasimishwa?

By International Federation for Human Rights (FIDH) / Eric Mirguet / Arnold Tsunga, on 8 September 2020



Katika hoja zinazotumika sana kutetea adhabu ya kifo ni kuwa inasaidia kupunguza uhalifu. Inaelezewa kuwa adhabu ya kifo inalinda jamii dhidi ya watu waliohatari na kuzuia wengine wasije wakafanya uhalifu. Hoja hizi zimethibitishwa kutokuwa na ukweli wowote. Je adhabu ya kifo inalinda jamii dhini ya uhalifu? Hailekei kuwa hivyo. Jamii zinazotumia adhabu ya kifo hazina ulinzi dhidi ya uhalifu kuliko zaidi ya zile jamii zisizotumia adhabu hiyo. Mahali ambapo kuna adhabu mbadala kama vile kifungo, ulinzi wa jamii, hautegemei kuwaondosha kimwili wahalifu. Zaidi ya hapo, inaweza kuelezwa kuwa tahadhari zinazochukuliwa kuzuia wanaosubiri, kuuwawa kujiua inaonyesha wazi kuwa kumuondosha kimwili mhalifu sio sababu ya msingi ya adhabu ya kifo.




Search